Watu
wamechukizwa nchini India na taarifa za madai ya mwanafunzi kubakwa
na kundi la wanaume watano, ambao pia walimbaka miaka mitatu
iliyopita.
Polisi
bado hawajamkamata mtu yeyote ingawa mwanafunzi huyo wa kike mwenye
miaka 21 alibakwa wiki iliyopita katika mji wa Rohtak katika jimbo la
kaskazini la Haryana.
Mwanafunzi
huyo wa kike alikuwa anafuatilia kesi iliyopo mahakamani dhidi ya
wanaume hao watano, wakati aliposhambuliwa na kubakwa siku ya
jumatano.
Mwanamke
huyo amesema alilazimishwa kuingia ndani ya gari, na kisha wanaume
hao walimkaba kooni na kumfanyia unyama huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni