Waziri
Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amezomewa alipohudhuria tukio la kukaa
kimya kwa dakika moja Jijini Nice kuwakumbuka watu 84 waliokufa kwa
tukio la kugongwa na lori.
Watu
waliomzomea Valls walimuita muuaji na kumtaka ajiuzulu, kabla ya
kuanza kwa kitendo hicho cha kukaa kimya kwa dakika moja katika
maeneo tofauti ya taifa hilo.
Mapema
kiongozi wa upinzani wa chama cha mrengo wa kati wa kulia ambaye ni
rais wa zamani Nicolas Sarkozy aliituhumu serikali kwa kushindwa
kutoa ulinzi kwa wananchi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni