John
Hinckley Jr, mtu aliyejaribu kumuua rais Ronald Reagan, anatarajiwa
kuachiwa kutoka kwenye hospitali ya vichaa mwezi ujao baada ya miaka
35.
Reagan
pamoja na walinzi wake watatu walijeruhiwa katika tukio hilo la
shambulizi la kutumia bunduki nje ya hoteli Jijini Washington Machi
1981.
Bw.
Hinckley hakutiwa hatiani kutokana na kuwa na matatizo ya akili na
kupelekwa kwenye hospitali ya wagonjwa wa akili iliyopo Jijini
Washington kwa ajili ya matibabu.
Hali ilivyokuwa siku ya tukio nje ya hoteli wakati huo Ronald Reagan akiwa rais wa Marekani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni