.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 22 Julai 2016

MTU ALIYEPANDIKIZWA MIKONO YOTE MIWILI ATARAJIA KUANZA TENA KUSHIKA VITU

Mtu wa kwanza nchini Uingereza kufanyiwa upasuaji wa kupandikiziwa mikono yote miwili, anatarajia kuanza kukamata tena glasi yake ya bia pamoja na kuvaa shati zenye batani.

Mtu huyo Chris King, 57, alipoteza vidole vyake na kubakia na viganja tu na vidole gumba katika ajali iliyotokana na mashine ya kukandamiza vyuma miaka mitatu iliyopita.

Sasa amekuwa mtu wa kwanza kupandikiziwa mikono yote miwili, na wa pili kufanyiwa upasuaji huo Uingereza. 
                    Mkono wake wa kushoto ulivyokuwa kabla ya kufanyiwa upandikizaji
                          Mkono wake wa kulia ulivyokuwa kabla ya kufanyiwa upandikizaji
Chris King akiwa na Profesa Simon Kay aliyeongoza jopo la upasuaji wa kupandikiza mikono

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni