Watu wapatao 55 wameuwawa kaskazini
mwa Pakistan na India katika mafuriko na maporomoko ya ardhi
yaliyosababishwa na mvua kubwa.
Polisi wamesema mafuriko katika
wilaya ya Chitral ya Pakistan yameharibu nyumba na msikiti na kuuwa
watu wapatao 30.
Watu wengine 25 wamefahamika kufa
katika mafuriko na maporomoko nchini India kwenye majimbo ya
Uttarakhand na Arunachal Pradesh.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni