Watu wapatao 125 wameuwawa na wengine
150 wamejeruhiwa katika milipuko inayodaiwa kufanywa na kundi la Dola
ya Kiislam (IS), polisi nchini Irak wamesema.
Gali lililokuwa na bomu limelipuka
karibu hoteli na eneo la manunuzi ya bidhaa katika wilaya ya kati ya
Karranda jana usiku.
Mtaa huo uliokuwa na harakati nyingi
za watu wakifanya manunuzi baada ya kufuturu wakijiandaa kumalizika
kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo.
Bomu lingine lililipoka baadaye
katika eneo linalokaliwa na waumini wa Kiislam wa Shia kaskazini mwa
Jiji la Baghdad na kuuwa watu watano.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni