Anaitwa Devota Sotel kutoka 91.0 Passion Fm Mwanza. Kwa muda mrefu amekuwa king'ang'anizi katika umahiri miongoni mwa watangazaji bora wa vipindi vya taarabu Jijini Mwanza na hata Kanda ya Ziwa.
Mambo yake si ya kitoto ukimsikiliza katika kipindi cha "Ambaa na Mwambao" kinachoruka 91.0 Passion Fm Mwanza kila siku jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa tano asubuhi hadi saa nane mchana.
Lakini pia jumamosi kuanzia saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili jioni na jumapili kuanzia saa kumi na moja jioni hadi saa mbili usiku.
Uwepo wake katika tasnia ya utangazaji hususani katika vipindi vya taarabu, kumeibua watangazaji wa taarabu wapya Mwanza ambao wamekuwa na ndoto za kufanya kazi kwa juhudi zaidi ili kumtoa Devota kwenye ubora wake alioukomalia kwa miaka mingi sasa.
Wapo watangazaji wengi wa taarabu ambao wanaibuka kwa kasi ya ajabu Jijini Mwanza na hivyo kuongeza mvuto kwa mashabiki wa taarabu Mwanza ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu ni mtangtazaji yupi wamsikilize na ni yupi wamuache.
Ubunifu pekee ndio utakaobainisha nani bora zaidi kwa mwaka huu 2016 na hivyo kumuondoa Devota kwenye ubora wake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni