.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 5 Julai 2016

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI DK. PALLANGYO AJIONEA ZOEZI LA UOKOAJI VIWANJA VYA SABASA

Ofisa wa Matukio ya Dharura wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Jeremia Ibambasi (kulia), akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo ya uokoaji kwa mtu aliyemeza hewa chafu katika kiwanda cha uchanjuaji dhahabu katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016 alipotembelea Banda la Wizara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo (kulia), akiangalia waokoaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) jinsi wanavyomsaidia mtu aliyevuta hewa chafu kwenye kiwanda cha uchanjuaji dhahabu nje ya banda la Wizara ya Nishati na Madini katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016 katika viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo mchana.
Waokoaji wakiondoka na majeruhi wakimpeleka lilipo gari la kubebea wagonjwa tayari kumpeleka mgonjwa Hospitali.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na maofisa mbalimbali wa wizara yake baada ya kwisha kwa zoezi hilo la uokoaji.

Hapa mfanyakazi wa Stamico, Paul Thobias (katikati), akionesha jinsi anavyosaidiwa na wataalamu baada ya kuvuta hewa chafu kiwandani.
Zoezi la kumtoa nguo majeruhi likiendelea. Nguo hizo zinahisiwa huwenda zikawa na hewa hiyo ya sumu.
Majeruhi akiendelea kutolewa nguo
Wananchi wakifuatilia zoezi hilo kwa karibu huku wengine wakiwa wameshika tama.
Hapa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na maofisa mbalimbali wa wizara yake baada ya kwisha kwa zoezi hilo la uokoaji.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na Ofisa wa Matukio ya Dharura wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Jeremia Ibambasi 

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni