.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 31 Julai 2016

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, ENG. RAMO MAKANI ATEMBELEA MAENEO YA HIFADHI YA MISITU NA WANYAMAPORI YENYE MIGOGORO MBALIMBALI MKOANI TABORA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambapo alifanya ziara ya kikazi ya siku nne na kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi ya Hifadhi ya Misitu na Wanyamapori yenye migogoro. Maeneo hayo ni Hifadhi ya Msitu wa Wembere (Wilaya ya Igunga), Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima (Wilaya ya Kaliua), Eneo la Jumuiya ya

Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole (Wilaya ya Skonge), Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi (Wilaya ya Skonge) na Msitu wa hifadhi wa Ilomero (Wilaya ya Nzega).
Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani akizungumza na baadhi ya wananchi waliovamia Msitu wa Hifadhi wa Wembere Wilayani Igunga hivi karibuni. Aliwataka wananchi hao kutii sheria za nchi na kusubiri maelekezo ya Serikali ambapo aliwaagiza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Igunga na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) kukusanya taarifa mbalimbali zinazohusu hifadhi hiyo na vijiji jirani ambapo zitatumika kumaliza mgogoro huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi wa waliovamia Msitu wa Wembere na kuweka makazi, Wilayani Igunga hivi karibuni. Alitoa maelekezo mbali kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania kwa ajili ya kukabili changamoto zilizopo katika hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Igunga pamoja na viongozi wengine kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto) akikagua maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Isawima Wilayani Kaliua hivi karibuni. Hifadhi hiyo ambayo imetengwa na vijiji 11 kwa ajili ya kuanzishwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima umevamiwa na wananchi kutoka maeneo ya nje ya vijiji hivyo na kuweka makazi, mifugo na kilimo jambo lililoikwamisha jumuiya hiyo kupewa kibali cha kurasimishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii. Eng. Makani alitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya ya Kaliua na Halmashauri kutumia mamlaka ya kisheria
waliyo nayo kuwahamisha wavamizi hao ili jumuiya hiyo iweze kuanzishwa.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mtapenda, Wilayani Kaliua wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtapenda, Wilayani Kaliua alipotembelea kuona changamoto wa Uhifadhi na kuweka utaratibu wa kuzikabili.
Mmoja wa wananchi waliovamia Hifadhi ya Isawima, Kaliua, Charles Msinda (kulia) akiiomba Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) iwafikirie kuwapa maeneo mbadala baada ya kuondoka katika Hifadhi ya Msitu huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati) akizungumza na viongozi wa Chama (CCM) na Serikali Wilayani Skonge. Kulia kwake ni mkuu wa Wilaya hiyo, Peres Boniface.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na jamii wa wavuvi wa Mto Koga, Wilayani Skonge ikiwa na hatua ya kusuluhisha mgogoro kati yao na muwekezaji, Muhsin Abdllah “Shein” ambaye ni Mkurugenzi wa Northern Hunting. Eng. Makani aliwataka viongozi wa Wilaya na Halmashauri kukaa pamoja na muwekezaji huyo na wadau mbaimbali kwa ajili ya kamaliza mgogoro huo. Aliwata viongozi hao kuangaliwa upya vibali vinavyotolewa kwa wavuvi hao ili idadi yake ilingane na ukubwa na mahitaji ya Mto huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akisikiliza malalamiko kutoka kwa muwekezaji ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Northern Hunting, Muhsin Abdallah (kushoto) aliyewekeza katika kitalu cha uwindaji kwenye Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole Wilayani Skonge.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ipembampazi, Wilayani Skonge Tabora. Wananchi hao wameiomba Serikali iwamegee eneo la hifadhi kwa ajili mradi wa kilimo cha umwagiliaji, Uluwa, Hifadhi ya Msitu ambao upo chini ya Halmashauri ya Wilaya Kaliua. Eng. Makani alitoa maelekezo mbalimbali kwa Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya na Mkoa ikiwa ni pamoja kuangalia taratibu za kisheria na kimazingira juu ya uwezekano wa ombi hilo na kuliwasilisha Wizarani kwa ajili ya hatua zaidi. (Picha na Hamza Temba – WMU – www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni