Zlatan
Ibrahimovic anaamini kuwa Manchester United itakuja kufanya mambo
makubwa baada ya kufunga kwa tik taka katika mchezo wake wa kwanza
akiwa na timu hiyo katika mchezo wa kirafiki.
Ibrahimovic,
34, alifunga goli hilo kwa staili hiyo ambayo hupenda kufunga magoli
yake mara nyingi baada ya kukutana na krosi ya Antonio Valencia huku
United ikiibuka na ushindi wa 5-2 dhidi ya Galatasaray.
Katika
mchezo huo hadi mapumziko Galatasaray ilikuwa ikiongoza kwa magoli
2-1 kupitia kwa Sinan Gumus na Bruma, lakini United walibadili
matokeo baada ya Wayne Rooney kufunga mawili, Marouane Fellaini na
Juan Mata moja kila mmoja.
Zlatan Ibrahimovic akifunga goli la kwanza kwa tik taka katika mchezo huo wa jana usiku
Wayne Rooney akiwa amepiga mpira ulioenda kujaa wavuni na kuandika goli la pili kwa Man U
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni