Mwanamichezo huyo Segovia Víctor
Barrio, 29, aliumizwa vibaya na ng'ombe huyo katika onesho ambalo
lilikuwa linarushwa moja kwa moja kwenye televisheni katika mji wa
Teruel huko Aragon, Mashariki mwa Hispania.
Mkewe aliyeshutushwa mno na tukio
hilo Raquel Sanz, alikuwa miongoni mwa watazamaji walioshuhudia janga
hilo katika mchezo wa kupigana na ng'ombe, wakati wachezaji wenzake
wakikimbia kujaribu kumuokoa.
Ng'ombe dume likimpiga pembe Segovia Víctor
Barrio na kumuangusha chini
Wapiganaji wengine wa mchezo huo wakijaribu kumnusuru mwenzao waliyelala na kupoteza kabisa fahamu
Segovia Víctor
Barrio akiwa amebebwa na wenzake ili kumuondoa uwanjani hata hivyo alishapoteza maisha
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni