.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 10 Julai 2016

LINDI SEKONDARI YATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO

                                                                                  Na Abdulaziz Video,Lindi

Shule ya Sekondari ya Lindi imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo tarehe 10/07/2016. Moto huo ambao ulianza majira ya saa saba usiku na Uliweza Kudhibitiwa kutoleta Athari zaidi baada ya Jeshi la Polisi, Zimamoto na Wananchi kushirikiana kwa pamoja na kufanikiwa kuudhibiti saa Moja Asb Ya Leo

Mpaka moto huu ulipodhibitiwa mali zifuatazo zilikuwa tayari zimeshaungua:-

· Madarasa tisa yameungua,ambapo matano yameungua pamoja na samani zilizokuwa ndani na mengine manne ni majengo peke yake Vifaa viliwahi kuokolewa na wananchi.

· Ofisi nne za walimu.

· Maabara mbili za kemia na fizikia zimeungua kwenye paa tu, hivyo samani za ndani hazijaungua.

· Takribani madawati zaidi ya 300 yameteketea kwa moto.

Majengo mengine ya shule yapo salama yakiwemo mabweni. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amewaomba wananchi na uongozi wa shule kuwa watulivu wakati Uongozi wa Mkoa Ukitafuta namna ya Kusaidia Wanafunzi Kuendelea na Mafunzo baada ya kufunguliwa kwa Shule hiyo kesho tr 11/07/2016

Aidha, Mkuu wa Mkoa amewashukuru wananchi wote waliojitokeza kuuzima moto huo kwani haikuwa kazi rahisi, pia amewashukuru polisi na jeshi la zimamoto kwa jitihada walizochukua katika kuudhibiti moto huo.

Kwa sasa inafanyika tathmini ya mali zilizoteketea kutokana na moto huo sambamba na uchunguzi wa chanzo cha moto. Taarifa kamili ya uchunguzi na tathmini itatolewa pindi itakapokamilika.

Katika Hatua Nyingine Mtu Mmoja alietaka Kuipa Komputa Mpakato katika tukio Hilo amekamtwa na Polisi Baada ya Wananchi kuanza Kumpa Adhabu.
 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni