.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 20 Julai 2016

NI DHIDI YA MTIBWA SUGAR JULAI 30 – MBEYA CITY COUNCIL FC

IMG-20160719-WA0035 
SIKU kadhaa baada ya kuanza kwa kambi ya mazoezi kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya tayari imethibitishwa kuwa kikosi cha Mbeya City fc kitasafiri mpaka mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri julai 30.

Kwa mujibu wa kiongozi wa Kanisa la Faith Baptist, Mch Jerry Wyatt ambaye ndiye mwandaaji na msimamizi mkuu wa mchezo huo,maandalizi yote ya mechi hiyo ya kirafiki itakayoambatana na tamasha kubwa la mahubiri ya neno la Mungu tayari yamekamilika ikiwa ni pamoja na timu zote kuthibitisha kuhudhuria.

“Maandalizi yote yamekamilika, timu zote zimethibitisha kushiriki katika mchezo huo ambao utaambana na mahubiri ya neno la Mungu kwenye uwanja wa Jamhuri, naomba watu wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia mchezo mzuri wa kirafiki kutoka kwa timu hizi mbili pia kupata mahubiri mazuri ya neno la Mungu sambamba na matukio mengine mengi” alisema.
1-family-photo-2014-crop-u11962 
Mch Jerry Wyatt akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake.

Akiendelea zaidi Mch Jerry alisema kuwa kwenye tamasha hilo la neno la Mungu na mchezo wa kirafiki wa soka hakutakuwa na kiingilio chochote kwa watakaofika kwenye uwanja wa Jamhuri na kwa wale watakaopata nafasi wanakaribishwa kuhudhuria ibada kwenye kanisa la Faith Baptist lililopo Kola B siku jumapili ya julai 31.

“Hakutakuwa na kiingilio, pia wale watakaopata nafasi nawakaribisha kuhudhuria ibada kwenye kanisa letu siku ya Jumapili siku ambayo pia tutatoa zawadi mbalimbali kwa timu za soka zaidi ya 40 za mjini hapa (Morogoro) kwa maana hiyo litakuwa jambo jema watu wote wakihudhuria”

Hii ni mara ya pili kwa Mtibwa na City kucheza mchezo wa kirafiki ulioandaliwa na Kanisa hilo awali ikiwa ni msimu uliopia ambapo timu hiyo kutoka Manungu iliibuka na ushindai wa bao 1-0 lililofungwa kipindi cha pili na Mohamed Ibrahim

City inatarajia kuondoka Mbeya Julai 28 tayari kwa mchezo huo uliopangwa kupigwa siku jumamosi ya mwisho wa mwezi huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni