Baba
wa watoto watatu nchini Uingereza inaaminika amemuuwa mkewe na binti
yake kwa kutumia bunduki kabla na yeye kujigeuzia mtutu na kujiuwa
katika mauaji yaliyotokea nje ya bwawa la kuogelea.
Baba
huyo Lance Hart, 57, inaaminika alimuua mkewe Claire Hart, 50, na
binti yake Charlotte Hart, 19, majira ya saa tatu asubuhi, katika
eneo la maegesho ya magari ya kituo cha The Castle Leisure huko
Spalding, Lincolnshire.
Watoa
huduma za dharura waliitwa baada ya waogeleaji na maafisa wa kituo
hicho kusikia milio ya risasi, kabla ya kubaini mwili wa mwanaume
mmoja pamoja na miili ya wanawake katika eneo la maegesho.
Magari ya polisi na magari ya kutoa huduma za dharura yakiwa katika eneo la tukio la mauaji hayo
Magari ya polisi na magari ya kutoa huduma za dharura yakiwa katika eneo la tukio la mauaji hayo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni