Alhamisi, 14 Julai 2016
PICHA ZA WAZIRI MKUU MAJALIWA AKIKAGUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIGAE CHA GOODWILL CERAMIC CHA MKURANGA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati akikagua ujenzi wa kiwanda cha vigae cha Goodwill Ceramic kwenye kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga Julai 13, 2016,Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na kulia ni Balozi wa China nchini, Dkt Lu Youqing.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wapili kulia) kwa ajili ya madawati wakati alipokagua ujenzi wa kiwanda cha vigage cha Goodwill Ceramic kinachojengwa katika kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga Julai 13, 2016. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandishi Evarest Ndikilo na kulia ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akipongezana na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega baada ya kupokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa Balozi wa China Nchini, Dkt. Lu Younqing kwa ajili ya madawati baada ya kukagua ujenzi wa kiwanda cha vigae cha Goodwill Ceramic kilichopo katika kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga Julai 13, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumzana Balozi wa China Nchini , Dkt. Lu Youqing (wapili kulia) , Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo (kushoto) baada kukagua ujenzi wa kiwanda cha vigae cha Goodwill na kuzungumza na wananchi kwenye kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga Julai 13, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Mtopa baada kuwa kuwasili mjini Lindi Julai 13, 2016 kwa ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mama Salima Kikwete, mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne baada ya kuwasili mjini Lindi kwa ziara ya kikazi Julai 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni