Paul
Pogba ameashiria kunukia Manchester United kwa uhamisho mnono wa
paundi milioni 100, kwa kutia saini yake kwenye jezi ya Manchester
United yenye jina lake ikiwa na namba sit iliyokuwa imevaliwa na
shabiki.
Shabiki
huyo wa Manchester United, Jonathan Perkins alikuwa akisherehekea
miaka 18 ya kuzaliwa akiwa mapumzikoni Jijini Los Angeles huku akiwa
amevaa jezi hiyo iliyoandikwa 'Pogba 6'.
Na
kwa mshangao shabiki huyo kijana alikutana na Pogba ambaye naye yupo
mapumzikoni wakati akitembe kwenye mitaa ya California na kumfuata na
kuandika saini yake nyuma ya jezi hiyo.
Paul Pogba akiwa amepozi katika eneo la Universal Studios Jijini Los Angeles Marekani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni