.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 30 Julai 2016

WAZIRI NAPE AONGOZA MAPOKEZI YA MWILI WA JOSEPH SENGA AIRPORT DAR

Waombolezaji miongoni mwao wakiwemo waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa MpigaPicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaamm jana, ktuoka nchini India ambako alipatwa na mauti. Wa pili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye pia alifika kwenye mapokezi hayo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Senga wakiwa Uwanja wa Ndege wakisubiri wa mpendwa wao. (Picha zote na Kamanda Richard Mwaikenda; Kamanda wa Matukio.
Maofisa wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Mizigo Uwanja wa Ndege, Swisport wakiutoa nje jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga.
Waombolezaji wakiuweka mwili wa marehemu Senga kwenye gari tayari kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wanachama wa Press Photographers Tanzania wakishiriki kuingiza kwenye gari jeneza la mwili wa wa aliyekuwa mpiga picha za habari Tanzania, marehemu Senga.
Dada wa marehemu Joseph Senga, Yunista Senga akilia kwa uchungu alipoona jeneza lenye mwili wa kakake, Joseph Senga.
Baadhi ya waombolezaji wakiwemo wapigapicha za habari wakiondoka Uwanja wa Ndege baada ya kuupokea mwili wa aliyekuwa mpiga picha mwenzao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni