Mwamamuziki
wa DR Congo Koffi Olomide amekamatwa kwa kumshambulia mwanamke katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
Koffi
Olomide amekamatwa jana usiku baada ya kufanya mahojiano ya moja kwa
moja na televisheni moja kubwa nchini Kenya, kufuati IGP Joseph
Boinnet kuamuru akamatwe.
Igizo
hilo la IGP Boinnet linafuatia video iliyosambaa kwenye mitandao ya
jamii ikimuonyesha mwanamuziki huyo akimpiga teke mwanamke mmoja
alipowasili JKIA.
Msanii
huyo nyota wa muziki wa Rumba aliwasili Jijini Nairobi majira ya saa
12 asubuhi kwa ajili ya onyesho lake linalongojewa kwa hamu
litakalofanyika Bomas of Kenya leo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni