Shambulizi
la kutumia bunduki Jijini Munich katika duka la bidhaa lililouwa watu
tisa limefanywa na mtu mmoja mwenye silaha ambaye naye alijiuwa,
polisi wa nchini Ujerumani wamesema.
Polisi
wameviambia vyombo vya habari kuwa mtuhumiwa aliyetekeleza shambulizi
hilo ni kijana wa miaka 18 mwenye Uraia wa Ujerumani na Iran ambaye
alikuwa akiishi Munich, hata hivyo haijajulikana dhamira ya
shambulizi hilo.
Katika
shambulizi hilo watu 16 walijeruhiwa na watatu miongoni mwao wakiwa
mahututi, huku msako ukianzishwa kufuatia ripoti kuwa zaidi ya watu
watatu wenye silaha walihusika na shambulizi hilo.
Mwili wa mtu aliyeuwawa kwa kupingwa risasi ukiwa umefunikwa kwa shuka jeupe
Kituo cha matibabu ya dharura kikiwa kimejengwa kwa muda ili kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni