Usain
Bolt ameonyesha kuboreka afya yake kabla ya michuano ya Olimpiki
mwezi ujao, baada ya kushinda mbio za mita 200 katika uwanja wa
Olimpiki wa London.
Bingwa
huyo wa Olimpiki mara sita alitumia muda wa sekunde 19.89, akiwa
mbele ya mwanariadha wa Panama Alonso Edward aliyeshika nafasi ya
pili.
Muingereza
bingwa wa medali ya fedha ya Jumuiya ya Madola Adam Gemili alishika
nafasi ya tatu akitumia muda wa sekunde 20.07.
Uwezo
wa Bolt kufanya vyema ulikuwa ukitiliwa shaka baada ya kutoweza
kushiriki majaribio ya kufuzu kushiriki michuano ya Olimpiki,
kutokana na jeraha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni