Kapteni
wa Uingereza Wayne Rooney amesema chama cha soka Uingereza FA
kimefanya uteuzi mzuri kwa kumchagua kocha Sam Allardyce kukinoa
kikosi cha taifa hilo.
Allardyce,
61, amesaini mkataba wa awali wa miaka miwili baada ya Chama cha Soka
Uingereza kukubali kuilipa fidia klabu ya Sunderland.
Mshambuliaji
huyo wa Manchester United, Rooney ambaye anaongoza kwa kuifungia
magoli mengi timu ya taifa alikuwa katika kikosi kilichotolewa katika
michuano ya Euro 2016.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni