Polisi
wa mji wa Florida wamempiga risasi na kumjeruhi mwanaume mweusi
mwenye matatizo ya kujieleza, ambaye husaidia watu wenye matatizo ya
viungo.
Mwanaume
huyo Charles Kinsey, ambaye anafanya kazi ya kusaidia walemavu,
ameiambia televisheni ya WSVN alikuwa akimsaidia mgonjwa aliyekuwa
akizurura katika jengo.
Picha
iliyopigwa kwa simu ya mkononi inamuonyesha Kinsey akilala chini na
kunyoosha mikono yake hewani, na mgonjwa wake akiwa amekaa barabarani
katika kiti maalum.
Tukio
hilo linafuatia wiki kadhaa za ghasi zilizohusisha polisi nao kuuwawa
kwa kupigwa risasi kufuatia matukio ya polisi kuwauwa kwa kuwapiga
risasi wanaume wawili weusi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni