JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti :
www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi
anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi
katika Mkoa wa Songwe.
Uhamisho
wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya
Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya
aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake
utenguliwe kutokana na sababu binafsi.
Bw.
Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa
viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini
Dar es salaam.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
07
Julai, 2016
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni