Mabweni
karibu ya shule tano yamechomwa moto jana usiku nchini Kenya na
kuongeza idadi ya mamia ya taasisi za elimu zilizoripotiwa kutokea
matukio ya moto katika kipindi cha miezi michache.
Moto
wa jana usiku umetokea kwenye shule za Sekondari za Giakaibii huko
Nyeri, Shule wasichana ya Merti huko Isiolo, shule ya mchanganyiko ya
Adega ya Homa Bay, St Stephen iliyopo Narok pamoja na shule ya
Sekondari ya St Patrick iliyopo Iten kaunti ya Elgeyo-Marakwet.
Kufuatia
mfululizo wa matukio hayo chama kikuu cha walimu nchini Kenya
kimeitaka serikali kuzifunga mapema shule kabla ya wakati wa likizo
kufika ili kuwaepusha wanafunzi na msongo wa mawazo juu ya uwezekano
wa kutokea moto mashuleni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni