Kocha
Pep Guardiola amepiga marufuku wachezaji wenye vitambi kushiriki
mazoezi ya kikosi cha kwanza cha Manchester City, na kuzuia ulaji wa
vyakula vinavyonenepesha.
Kocha
huyo hakupoteza muda kutoa miongozo yake ya kinidhamu kwa wachezaji
wa timu yake hiyo mpya, miongozo ambayo pia aliitumia akiwa na
Barcelona na Bayern Munich.
Miongoni
mwa wachezaji waliogizwa kupunguza unene ni pamoja na Samir Nasri,
ambaye sasa anakazi ya kupunguza uzito kilo kadhaa ili ajiunge na
wenzake wa kikosi cha kwanza.
Samir Nasri hana jinsi zaidi ya kufanya mazoezi zaidi na kupunguza milo inayonenepesha ili kuweza kuwa katika kikosi cha kwanza cha Manchester City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni