Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa masuala ya Kidiplomasia katika Taasisi ya Aga Khan, Balozi Arif Lalani alipotembelea Wizarani kwa ajili ya kujitambulisha na kueleza nia ya Taasisi hiyo ya kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katkati miradi ya maendeleo hususan katika sekta ya elimu
Sehemu ya wageni walioambatana na Balozi Lalani (hayupo pichani). Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya
Aga Khan nchini, Bw. Amin Kurji nao wakisikiliza mazungumzo kati ya Balozi Muombwa na Balozi Lalani (hawapo pichani).
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Ramla Khamis (kushoto), pamoja na Afisa Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Hellen Mgeta wakifuatilia mazungumzo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni