Uturuki
imewasimamisha kazi maafisa elimu 15,200 kwa tuhuma za kuwa na
uhusiano na kiongozi wa kidini aishiyeukimbizini anayelaumiwa kwa
kuhusika na jaribio la mapinduzi la wiki iliyopita.
Wizara
ya Elimu imetoa tangazo hilo lakini halijaeleza wazi ni wakina nani
haswa ndio waliosimamishwa kazi.
Hatua
hiyo imekuja wakati Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim akiapa
kuwasaka wafuasi wa kiongozi wa Kiislam Fethullah Gulen hadi katika
mizizi yao.
Gulen,
ni kiongozi wa kidini ambaye anaishi nchini Marekani na amekanusha
kuhusika na mapinduzi hayo yaliyoshindwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni