Mke
wa Donald Trump, Melania, amepanda jukwaani katika siku ya kwanza ya
mkutano wa kitaifa wa chama cha Republican, na kujikuta akikabiliwa
na tuhuma za kukopi sehemu ya hotuba ya Michelle Obama.
Watu
waliokuwa wanafuatili hotuba ya Melania Trump, walibaini kufanana kwa
shehemu ya hotuba hiyo na ile aliyoitoa Bi. Michelle Obama katika
hotuba yake ya mkutano wa kitaifa wa chama cha Democratic mwaka 2008.
Hotuba
ya Bi. Trump ilimsifia mumewe kuwa ni mtu mnyenyekevu na ni mtu
anayeweza kupigania taifa la Marekani. Timu ya Bw. Trump imejitetea
kuwa Bi. Trump alitumia maneno yanayotumika kawaida mara zote.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni