Kocha Carlo Abcelotti amechochea
homa ya mchezo wa nusu fainali ya Euro 2016, baada ya kusema kuwa
Gareth Bale na Cristiano Ronaldo wamekuwa wakishindana wakati wa
mazoezi ndani ya klabu yao ya Real Mardid.
Iwapo ushindani huo wa wachezaji hao
upo hivyo wakiwa ndani ya klabu moja, leo usiku itakuwaje wakati
wawili hao wakiwa na timu zao za taifa za Wales na Ureno kuwania
kufuzu faiali za michuano ya Euro 2016.
Hakika kwa wapenzi wa soka duniani
leo macho yao watayaelekeza Jijini Lyon, Ufaransa ili kupata jibu la
kitendawili kigumu cha nani mkali kati ya Gareth Bale akiwa na Wales
ama Cristiano Ronaldo akiwa na Ureno.
Cristiano Ronaldo akiwa anaiwakilisha Ureno
Gareth Bale akishangilia ushindi akiwa na Wales
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni