Vikosi
vya zimamoto vya California vinahangaika kuudhibiti moto ambao
umeteketeza nyumba 18 na kutishia nyingine mia moja katika eneo la
mlimani kaskazini mwa Los Angeles.
Moto
huo wa nyika umetapakaa katika eneo la zaidi ya hekari 22,000, na
wakazi wa nyumba karibu 1,500 huko Santa Clarita wamehamishwa.
Mwili
wa mtu mmoja umepatikana kwenye gari lililoungua moto, ingawa
haijafahamika mara moja iwapo kifo chake kimetokana na moto.
Gari la Zimamoto likiwa linazingirwa na miale ya moto wakati vikosi vya Zimamoto vikipambana na moto huo
Askari wa kikosi cha Zimamoto akipambana kuuzima moto huo katika eneo la Mlimani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni