Timu
ya taifa ya Wales imetinga nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 kwa
mara ya kwanza baada ya kupambana kiume na kuifunga Ubelgiji kwa
jumla ya magoli 3-1 katika mchezo uliochezwa huko Lile, Ufaransa.
Alikuwa
Radja Nainggolan aliyeifanya Ubelgiji kuongoza kupata goli kwa shuti
kali la yadi 25, hata hivyo kapteni wa Wales Ashley Williams
alisawazisha kwa mpira wa kichwa kufutia mpira wa kona na kufanya
kipindi cha kwanza kuisha kwa sare ya 1-1.
Wales
walipata furaha pale Hal Robson-Kanu, mshambuliaji asiye na klabu
alipopachika goli na kuwafanya kuongoza kwa magoli 2-1, huku Sam
Vokes aliyetokea benchi akipachika goli la tatu.
Kwa
ushindi huo Wales sasa watakutana na Ureno katika mchezo wa nusu
fainali, itakayowakutanisha washambuliaji wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo na Gareth Bale.
Hal Robson-Kanu akipiga mpira uliozaa goli la pili kwa Wales
Sam Vokes akiwa juu baada ya kuupiga mpira kwa kichwa ulioandika goli la tatu kwa Wales
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni