Mkuu mpya wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo akiongea na wadau mbalimbali waliouthuria katika sherehe za kuapishwa kwa wakuu wa wilaya wapya wa wilaya tano zilizopo mkoa ndani ya mkoa wa Arusha ,ambapo mkuu huyu wa wilaya aliwataka wadau mbalimbali pamoja na wananchi kumpa ushirikiano katika kufanya kazi ,huku akisisitiza kuwa swala ya siasa pamoja na mambo ya kisiasa yameisha sasa hivi ni muda wa kufanya kazi tu(Habari picha na Woinde Shizza, Arusha )
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha walioapishwa Jumamosi wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Felexs Ntebenda pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Adolfu Mapunda nje ya jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa
Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Geofrey Chongolo akikaribishwa rasmi na mmoja wa viongozi wa CCM wilayani humo kwa kupewa shuka la Kimasai hii ikiwa ishara ya kuwa wilaya yake ina wananchi wengi wa kabila la kimasai na Kiarusha ambao ni wafugaji
Aliekuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Wilson Nkambaku akiongea na wananchi wa mkoa wa arusha pamoja na baadhi ya viongozi wakati wa sherehe za kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya ambao wameteuliwa na rais Magufuli,ambapo mkuu huyu wa wilaya aliwaomba wananchi pamoja na wafanyakazi wa serekali kuwapa ushirikiano wa kutosha viongozi walioteuliwa huku akimshukuru rais magufuli kwa kumpa ushirikiano katika kipindi cha miezi nane aliyefanya nae kazi huku akimuaidi kuendelea kutoa ushirikiano katika serekali yake pamoja na chama kwa ujumla
Baadhi ya wananchi waliouthuria sherehe izo za kuapishwa wakuu wapya wa wilaya
huku wa pili akiwa ni mkuu wa wilaya ya monduli Idd Hassan Kimanta mara wakiwa wameketi wakisiliza hutuba ya mkuu wa mkoa wa Arusha (hayupo pichani )mara baada ya kuapishwa rasmi hii leo baadhi ya wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara ,viongozi wa dini na wananchi waliouthuthiria katika sherehe za kuapishwa wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Arusha Mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexander Pastory Mnyeti akila kiapo cha utiii mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha hii leo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni