Seneta
wa Texas Ted Cruz amezomewa baada ya kushindwa kumuunga mkono Donald
Trump kama mgombea urais kwa chama cha Republican, wakati akitoa
hotuba yake kwenye mkutano mkuu wa kitaifa wa chama hicho huko
Cleveland.
Katika
hotuba yake hiyo Cruz aliishia kumpongeza Trump ambaye alikuwa ni
mshindani wake mkuu katika kinyang'anyiro cha kupata kura za awali za
wanachama wa chama hicho cha Republican.
Kundi
la wanachama wenye hasiri walisikika wakisema “Tunamtaka Trump”,
na kuongeza “Muidhinishe”, wakati Cruz alipokuwa akikaribia
kumalizia hotuba yake hiyo katika mkutano huo.
Seneta Ted Cruz akiwapungia mkono wanachama wa Republican baada ya kukamilisha hotuba yake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni