Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mapema leo mchana kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika uliomalizika hivi karibuni nchini Rwanda.
Katika mkutano huo Mhe. Waziri alielezea mambo mbalimbali yaliyojadiliwa katika Mkutano huo ikiwemo uala zima la Haki za Wanawake katika kufanya maamuzi kupata nafasi za Uongozi na kushirikishwa kwenye utatuzi wa migogoro mbalimbali Barani Afrika.
Kaulimbiu ya mkutano huo ilihusu "Haki za binadamu hususan za Wanawake" Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizarani, Bi. Mindi Kasiga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni