Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela akipokea kitabu toka kwa Bwana Daniel El Noshokaty ambaye alikabidhi vitabu kwa kila mwanafunzi kwa ajili ya kujisomea.
MKUU wa wilaya ya Iringa,Richard Kasesela leo amefungua kongamano la wanafunzi wa shule za sekondari kujadili maendeleo na matumizi ya rasilimali.
Kongamano hilo liliandaliwa na umoja wa walimu wa masomo ya Uraia CETA wakishirikiana na KAS -taasisi ya kujerumani. Katika hotuba yake, mkuu wa wilaya alisistiza kuwa rasilimali kubwa inayotakiwa kufanyiwa kazi ni Binadamu.
Alisema " binadamu akijengewa uwezo anaweza kubadilisha rasilimali hizi ziwe na faida kwa maisha yake na wengine". Mkuu wilaya alisistiza suala la nidhamu kama msingi wa maisha, upendo na udailifu vinaleta mabadiliko katika maisha ya mwanadamu.
Naye Mwakilishi wa KAS, Bwana Daniel El Noshokaty akimkaribisha Mkuu wa wilaya alisema, Taasisi ya KAS imeanza toka mwaka 1964 ikiwa na kazi ya kuelimisha wananchi juu ya elimu ya uraia hapa Tanzania, na imetoa vitabu vingi kuhakikisha Watanzania wanapata uelewa wa elimu hiyo.
Kwa Iringa wataendelea kuelimisha wanafunzi watambue fursa zilizopo katika rasilimali nyingi. Kongamano la siku moja lilikuwa na na mada zenye kutambua uwezo wa nchi katika kuleta thamani kwa rasilimali zilizopo Tanzania hasusan Iringa.
Shule za Lugalo, St Joseph, Kleruu, Kwelu, Highland na Mkwawa zililishirki katika kongamno hilo.
Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kaseselaakiongea na wanafunzi hao mara baada ya kupkea vitabu kwa kila mwanafunzi kwa ajili ya kujisomea.
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni