Kocha
Pep Guardiola amekaribishwa kwa kipigo wakati aliporejea katika dimba
la Allianz Arena, katika mchezo wake wa kwanza kama kocha wa
Manchester City dhidi ya timu yake ya zamani ya Bayern Munichi.
Katika
mchezo huo uliopigwa jana Guardiola aliyeonekana mchangamfu mno baada
ya kukaribishwa vyema na klabu yake hiyo ya zamani, na mara kwa mara
alionekana akitoa maelezo kwa wachezaji aliokuwa anawabadilisha.
Goli
pekee katika mchezo huo lilifungwa na Erdal Ozturk katika dakika 14
kabla ya kumalizika kwa mchezo huo, kwa shuti lililougonga mguu wa
Gael Clichy na kumpoteza mahesabu kipa wa Manchester City.
Mchezaji Erdal Ozturk akiachia shuti lililozaa goli pekee la Bayern Munich
Pep Guardiola akitoa maelezo kwa Yaya Toure kabla ya kumuingiza dimbani
Mshambuliaji wa Bayern Munich Frank Ribery akiangalia jezi yake iliyochanika
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni