Kocha
Sam Allardyce anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa
ya Uingereza, huku uthibitisho rasmi ukitarajiwa kubainika hii leo.
Kocha
Allardyce ataachana na klabu ya Sunderland baada ya miezi tisa katika
klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Allardyce,
61, anachukua nafasi ya kocha Roy Hodgson, ambaye alijiuzulu mwezi
Juni baada ya kushindwa na timu ya Iceland katika hatua ya 16 bora ya
miuchuano ya Euro 2016.
Allardyce,
ambaye aliwahi kuzinoa West Ham, Newcastle na Bolton, aliongea na
Chama cha Soka cha Uingereza, (FA) wiki iliyopita na amempiku kocha
wa Hull, Steve Bruce.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni