.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 12 Julai 2016

WAZIRI MAHIGA APOKEA MSAADA WA MADAWATI 105 KUTOKA JUMUIYA YA MABOHORA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza zoezi la makabidhiano ya madawati kutoka Jumuiya ya Mabohora iliyopo hapa nchini, jumuiya hiyo imechangia jumla ya madawati 105 yenye thamani ya shilingi milioni kumi.

Hii ni katika kuiunga mkono Serikali kwenye zoezi la kuchangia madawati nchi nzima lililo tangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Madawati hayo yametengenezwa hapa nchini na Kampuni ya Jambo.

Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora, Mhe. Shehe Zainuddin Adamjee naye akizungumza na waandishi wa habari kwenye makabidhiano ya madawati.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini Waziri Mahiga
Sehemu ya wawakilishi wa Jumuiya hiyo wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Mahiga
Waziri Mahiga akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya dawati kati ya yaliyotolewa na Jumuiya ya Mabohora. Wizara itakabidhi madawati hayo kwa Mamlaka husika kwa ajili ya kusambazwa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akiwa na Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Mabohora nchini, Mhe. Shekh Tayabali Hamzabhai ( (kushoto) na Shekh Zainuddin Adamjee, Makamu Mwenyekiti (kulia) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni