.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 30 Agosti 2016

BARAZA KUU LA CUF LIMEWASIMAMISHA UANACHAMA WANACHAMA KUMI NA MOJA

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazurui akizungumza na wandishi wa Habari katika Ofisi ya Chama hicho iliyopo Vuga Mjini Zanzibar wa kwanza (kushoto) Mkurugenzi Habari na Mawasiliano wa Chama Salum Bimani na wapili (kulia) Shaweji Mketo, Naibu Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi.

Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Chama cha Wananchi CUF wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Nassor Ahmed Mazrui.
Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF Shaweji Mketo akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wa chama hicho uliofanyika Ofisini kwao Vuga Mjini Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanazibar)
                                           Na.Rahma.Khamis/Kijakazi.Abdallah Maelezo Zanzibar
Chama cha Wananchi (CUF) kimemfukuza uwanachama Kaimu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wazee Shashu Legeye na kuwasimamisha uwanachama wanachama 11 kufukuzwa baada ya kusababisha vurugu la Mkutano Mkuu uliofanyika Agost 21 katika Ukumbi wa Ubungo Plaza Dar-essalam.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Vuga Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazurui amesema Baraza kuu la Uongozi la Taifa la Chama kimeamua kuchukua hatua za kinidhamu kwa Viongozi na wanachama waliohusika kuchochea vurugu hizo.

Amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya wanachama hao kutokuwa na uaminifu kwa chama na kukubali kurubuniwa na baadhi ya vyama vya siasa na kutumiliwa kufanya vurugu.

Aliwataja wanachama waliosimamishwa kuwa ni Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Magdalena Sakaya, Abdul Kambaya, Ashura Mustafa, Omar Muhina Masoud,Thomas Malima, Kapasha H. Kapasha, Maftaha Nachuma,Mohammed Habibu Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo. Rukiya Kassim Ahmed na Athumani Henku wamepewa karipio kali.

Mazrui amesema Baraza Kuu la Taifa la CUF limewateuwa wajumbe wengine wa Kamati ya Uongozi wakiwemo Julius Mtatiro kuwa Mwenyekiti wa CUF, Katani Ahmed Katani na Severina Mwijage kuwa Wajumbe .

Aidha Baraza Kuu limewateua Joran Basange kuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu kwa upande wa Tanzania Bara, Mbarala Maharagande kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mawasiliano kwa Umma hadi nafasi zitakapojazwa rasmi kwa mujibu wa sheria ya CUF.

Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu amewahakikishia wanachama na wapenzi wa CUF kuwa chama bado kipo imara na makini na hakitoyumbishwa kwa hila na njama za wasaliti.

Nae Naibu Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi Sheweji Mketo amesema kuwa wao wanafanyakazi ya siasa kwa kuwakomboa Watanzania na wamejipanga kuhakikisha wanachukua Dola uchaguzi wa 2020.

                                                     IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni