Profesa Julius Nyang'oro ni Mwalimu, mtaalam wa sayansi ya siasa na mwanasheria.
Amekuwa mwalimu tangu mwaka 1977 nchini Tanzania na hapa nchini Marekani.
Ni
mwandishi wa vitabu zaidi ya 14, vingi vikiigusia Tanzania kwa namna
moja ama nyingine. Moja ya vitabu alivyoandika, na ambavyo
vilimtambulisha zaidi kwa jamii ya waTanzania, ni kumhusu Rais mstaafu
Jakaya Mrisho Kikwete.
Ambapo ameandika vitabu viwili kumhusu.
Prof Nyang'oro alikuwa mkarimu sana kuungana nasi kwenye
kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu ya Agosti 29, 2016 kuzungumzia mambo
mbalimbali kuihusu Tanzania akiwa mwandishi, mwalimu, mtaalamu wa
mausala ya siasa na mwanasheria.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni