Robert
Lewandowski amefunga magoli matatu 'hat-trick' wakati Bayern Munich
ikiichakaza Werder Bremen kwa magoli 6-0 katika mchezo wao wa kwanza
wa ligi ya Bundesliga.
Mabingwa
hao watetezi wa ligi hiyo wanaonolewa na Carlo Ancelotti walipata
goli la kwanza safi katika dakika ya tisa kupitia kwa Xabi Alonso.
Kisha
mshambuliaji raia wa poland Lewandowski ndipo alipoanza kuonyesha
makali yake ya kucheka na nyavu baada ya kupita dakika akiunganisha
pande la Franck Ribery.
Xabi Alonso akiifungia Bayern Munich goli
Robert Lewandowski akifunga goli lake la tatu kwa mkwaju wa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni