Maombolezo
ya kitaifa yameanza nchini Italia kufuatia vifo vya watu wapatao 300,
ambao wamekufa kwa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea kwenye mikoa
ya eneao la milimani.
Waziri
Mkuu wa Italia Matteo Renzi anatarajia kuhudhuria mazishi ya kitaifa
kwa watu waliokufa huko Arquata, amboa ni moja ya miji iliyoathiriwa
vibaya na tetemeko la ardhi.
Hali
ya tahadhari imetangazwa katika maeneo yaliyodhurika na kiasi cha
fedha cha paundi milioni 42 kimeahidiwa kujenga upya majengo
yaliyoharibika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni