.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 29 Agosti 2016

CHAMA CHA WAAJIRI TANZANIA (ATE) CHAZINDUA TUZO YA MWAJIRI BORA 2016

pe1
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu tuzo za Mwajiri Bora 2016 zinazotarajiwa kutolewa mwezi Disemba mwaka huu. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za ATE,jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Mradi, Joyce Nangai.
pe2
Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Mradi, wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Joyce Nangai (kushoto) akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka.
pe3
Baadhi ya waandishi wa habari wakirekodi wakati Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk Aggrey Mlimuka akizungumza nao kuhusu tuzo za mwaka huu za Waajiri Bora zinazotarajiwa kutolewa baadae mwaka huu.

Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) leo kimezindua Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2016 kutambua Waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kibiashara.

Akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Aggrey Mlimuka alisema kwamba lengo kuu la Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka ni kutambua wanachama wenye sera nzuri za usimamizi wa rasilimali watu.

Alisema kuwa kwa miaka kadhaa tuzo hiyo imesaidia kuhamasisha wanachama kujikita katika kushughulikia masuala ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama msingi muhimu katika kumwezesha mwajiri kuwa na wafanyakazi wenye kukikidhi ushindani, wanaojituma na wenye furaha.

Aliongeza kuwa tuzo hiyo ilifuata mbinu za kisayansi na kitaalamu ili kuangalia umuhimu wa Rasilimali Watu katika makampuni ya kibiashara kuanzia makampuni makubwa kwa madogo na yale ya kati ili kuinua ujuzi na kuwa na wafanyakazi wenye kufanaya kazi kwa kujituma kama njia ya kutoa motisha kwa wafanyakazi ambao ndio msingi wa rasilimali watu.

Aliongeza kuwa EYA lilikuwa tukio muhimu linalofanywa na ATE kila mwisho wa mwaka tangu mwaka 2005. Alisema kuwa tuzo hiyo imekuwa maarufu hapa nchini katika muktadha wa biashara hasa kwa kuhamamasisha makampuni makubwa na madogo na ya ukubwa wa kati kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora ya kufanya biashara nchini.

Aliongeza kuwa tukio hilo la kutafuta mshindi limegawanyika katika makundi makuu mawili ambapo litaanza na kufanya utafiti kwa kutumia Mshauri Mwelekezi na hatua ya pili itakuwa ni hafla ya kutoa tuzo yenyewe kwa washindi ambalo litafanyika mwezi Desemba 2016.



“Tukio hili limegawanyika katika makundi mawili, ambapo hatua ya kwanza ni kufanya utafiti na hatua ya pili ni hafla ya kutoa tuzo kwa washindi,” alisema.

Aliwaomba pia Wanachama kushiriki kwa wingi ili kuweza kushindana na waajiri wengine kupitia shughuli wanazozifanya. Aliongeza kuwa kwa mwaka huu waajiri wataweza kujifunza kupitia kile kinachofanywa na makampuni mengine ili kuhakikisha wanakuwa na wafanyakazi wenye wanaojituma na wenye furaha katika kufanya kazi.

Dkt. Mlimuka alisema kuwa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2016, ilikuwa ya 9 tangu kuanza kwake na kuaongeza kuwa tuzo hiyo kwa mwaka huu itakuwa ya tofauti kulinganisha na zile zilizotangulia kwa kuwa itahusisha tuzo nyingine mbili mpya mojawapo ikipima Ushiriki wa Wafanyakazi ili kujua ni kwa kiasi gani wafanyakazi wanajihusisha na kazi wanazofanya, wanajitoa kwa ajili ya waajiri wao, na kama wana bidii katika utendaji kazi wao.

Alisema kuwa tuzo nyingine mpya ilikuwa ikiangalia umuhimu wa Usimamizi wa Vipaji na Kuviendeleza na lengo lake ni kuyawezesha makampuni kuvutia, kutunza, kutoa motisha na kuendeleza majhitaji ya wafanya kazi kwa sasa na siku za usoni

“Tumeanzisha tuzo mbili mpya kwa mwaka huu ili kuwawezesha waajiri kuboresha mazingira ya biashara kuhakikisha wafanyakazi wao wanashiriki kikamilifu katka utendaji kazi na hivyo kumwezesha mwajiri kupata na kuvutia waafanyakazi wenye ujuzi stahiki kwa manufaa ya sasa na siku za usoni,” alisema Dkt. Mlimuka.

Alisema kuwa tuzo hiyo imekuwa ikijikita katika kuangalia maeneo muhimu ya kusimamia Rasilimali Watu kama vile Uongozi na Utawala, Usimamizi wa rasilimali watu, Kusaidia na Kuwajibika kwa Jamii, Ubora na Uzalishaji, Kushirikisha Watu Wenye Ulemavu na Kujali Wafanyakazi.

Akizungumzia kuhusu namana ya kushiriki katika tuzo hiyo, Dkt. Mlimuka alishauri wanachama kushiriki kwa kujaza dodoso kupitia njia mojawapo kati ya njia tatu ambazo ni kwa njia ya umeme (Electronically), kwa njia ya mtandao (Online), au kwa kuwasilisha dodoso zilizojazwa kwa mkono.

Alikumbusha kuwa wanachama wwanaopenda kushiriki dodoso kupitia anuani ya: www.eya2016.co.tz ili kushiriki katka tuzo hii muhimu sana. Alisema kuwa mwisho wa kujaza dodoso za ushiriki itatakuwa Ijumaa tarehe 30 Septemba 2016.

Mwaka jana Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka ilifanyika kwa mafanikio makubwa ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Kassim M. Majaliwa (MB) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ushiriki uliongezeka kwa 100% kulinganisha na mwaka uliopita na kwa mwaka huu tunategemea idadi ya washiriki itaongezeka mara dufu. 


Makampuni mengi yalishiriki katika tuzo hiyo na baadhi ya washiriki walishinda tuzo hiyo na kati ya washindi hao alikuwa Tanzania Brewies Ltd (TBL), CCBRT, Kilombero Sugar Company, Social Security Regulatory Authority, Yakubu & Associates Chambers, Total Tanzania Ltd, TIGO Tanzania, CRDB Bank Plc na Geita Gold Mine. Kwa taarifa zaidi kuhusu EYA iliyopita tembelea www.eya.oc.tz. Mwaka huu tunategemea kuwa wanachama wengi zaidi watashiriki na wanasubiri tuzo hii kwa shauku kubwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni