.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 3 Agosti 2016

CHINA YAZINDUA DARAJA LA KIOO LA JUU YA MLIMA LENYE KUOGOPESHA

China imezindua eneo la kupita kwa miguu lililo juu ya mlima lililojengwa kwa vioo kando ya mlima kusini mwa nchi hiyo ambalo limekuwa kivutio cha watalii wenye roho ngumu kupita eneo hilo.

Daraja hilo la mzunguko kando ya mlima liitwalo 'Coiling Dragon Cliff', limezinduliwa Agosti mosi, kwenye Mlima Tianmen katika Mbuga ya Taifa ya Tianmenshan huko Zhangjiajie.

Tayari watalii wameanza kukaribishwa kuburudika na madhari hiyo ya daraja la urefu wa kutoka chini wa futi 4,600, urefu wa kutembea wa futi 330 na upana wa futi 5, ambalo humpa mtalii fursa nzuri ya kutazama.
             Mtu akiwa amelala kwenye daraja hilo akipigwa picha ya kumbukumbu
     Mwanamke akipita kwa hofu kwenye daraja hilo huku akishikilia eneo la mlima

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni