Mwanamuziki, Chris Brown, amekamatwa
kwa tuhuma za kumtishia mwanamke kwa kutumia silaha baada ya mwanamke
huyo kutoa taarifa hiyo polisi.
Mrembo huyo, Baylee Curran,
ameliambia gazeti la LA Times kuwa Brown alimuonyeshea silaha usoni
baada ya kushangaa mkufu wa madini wa rafiki yake.
Mwanamuziki huyo alitoka nje na
kukamatwa na polisi baada ya tukio hilo lililotokea siku ya jumanne.
Chris Brown amewahi kutiwa hatiani
mara kadhaa kwa kufanya fujo, ikiwemo shambulizi la mwaka 2009 kwa
aliyekuwa mpenzi wake Rihanna.
Chris Brown akiwa amenyanyua mikono juu
Polisi wakimsachi Chris Brown na rafiki yake
Mrembo Baylee Curran, anayedai kutishiwa maisha yake kwa mtutu wa bunduki na Chris Brown
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni