David Rudisha amekuwa mwanariadha wa
kwanza tangu Peter Snell wa New Zealand kutwaa mara mbili medali ya
dhahabu katika mbio za mita 800 katika michuano ya Olimpiki mwaka 1964.
Rudisha raia wa Kenya aliongoza mbio
hizo zikiwa katika umbali wa kilomita 300, baada ya Mkenya mwenzake
Alfred Kipketer kuongoza katika mzunguko wa kwanza.
Katika mbio hizo Rudisha alimaliza
kwa kutumia sekunde 42.15, mbele ya Taoufik Makhloufi wa Algeria na Mmarekani Clayton Murphy.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni