Timu ya wanaume ya Mpira wa Kikapu
ya Marekani imeonekana ikipata wakati mzuri wakati ikicheza mpira wa
wavu wa ufukweni huku wakiburudika kwa kunywa maji ya madafu nchini
Brazil.
Timu hiyo inayoshiriki michuano ya
Olimpiki huko Rio, jumapili ilipata ushindi finyu dhidi ya Australia
wa vikapu 100-97, ikiwa ni ushindi wa tatu mfululizo wa alama chache
baada ya kuishinda Australia kwa tofauti ya pointi 10 na Serbia
pointi 3 siku ya Ijumaa.
Wachezaji wa timu ya Kikapu ya Marekani wakijifurahisha kwa kucheza mpira wa wavu wa ufukweni na baadhi ya watu waliofika katika ufukwe kuwashuhudia
Mchezaji wa Mpira wa Kikapu wa Marekani, DeAndre Jordan akiwa ameshikilia dafu
Wachezaji wa Mpira wa Kikapu wa Marekani wakiwa wamekaa huku baadhi yao wakiwa na madafu mkononi




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni