Na Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi amezuru katika kituo cha Afya cha
Mlali kilichopo Katika Kata ya Mlali Wilayani humo kusikiliza kero
wanazokumbana nazo wakati wanapofika hospitalini kupatiwa tiba.
Huu ni muendelezo wa ziara za
kusikiliza kero za wananchi nakuzitatua kwa dhamira ya kupunguza na
kuziondoa kabisa kero ndogo ndogo ambazo zimesababishwa na wananchi
wenyewe ama watendaji wa serikali katika maeneo yote ya Wilaya
hususani sekta ya Afya.
Mara baada ya kuwasili katika kituo
hicho cha Afya alitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo majengo
mbalimbali, wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia
kwa kutokana na kujengwa chini ya kiwango huku likiwa na eneo Dogo
kiasi cha kupelekea kushindwa kuweka vitanda vya kutosha kwa ajili ya
wagonjwa.
Licha ya jengo hilo kujengwa chini
ya kiwango chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
kabla ya Mkuu huyo wa Wilaya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhudumu katika Wilaya hiyo.
Hata hivyo kufuatia kadhia hiyo Mhe
Ndejembi ameagiza Mkandarasi kutafutwa haraka iwezekanavyo ili aweze
kuhakikisha jengo hilo linarekebiswa upwa kwa kutumia gharama zake
mwenyewe.
Dc Ndejembi amemtaka mganga mkuu wa
Kituo cha afya Mlali kuhakikisha anasimamia vyema Mali na majengo ya
umma ili kuendelea kutoa huduma nzuri na zenye ufanisi kwa kila
Mtanzania anayefika katika Zahanati hiyo.
Kwa upande wa wananchi waliofika
kupatiwa huduma kutoka katika Kijiji cha Mlale na maeneo Jirani
wamesema kuwa huduma zinazotolewa katika Kituo hicho cha Afya zina
ahueni kubwa huku changamoto kubwa ikiwa ni uduni katika huduma za
chanjo kwa watoto kwani hawapati huduma hiyo kwa wakati.
Sambamba na hayo Dc Ndejembi
ameagiza kusimamiwa haraka na kutatuliwa kwa kadhia hiyo ili wananchi
wafurahie huduma bora zitolewazo katika vituo vya Afya sawia na
kuimarisha Afya zao ili kufanya Kazi kwa salama na kuitikia dhana ya
HapaKaziTu kwa vitendo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe. Deogratius Ndejembi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha afya Mlali
DC Ndejembi alipotembelea wodi wa wagojwa
DC Ndejembi akisisitiza jambo kabla ya kuondoka katika kituo cha afya Mlali
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni