Kurejea kwa Lionel Messi kuichezea
timu ya taifa, huenda kukacheleweshwa na kuwa majeruhi, lakini
wachezaji wenzake wa Argentina wanaonekana kutovunjika moyo kumkosa
nyota huyo.
Timu ya Barcelona imetangaza kwamba
Messi ameumia misuli ya paja lake la mguu wa kushoto, hivyo huenda
asicheze mchezo wa ujao wa kuwania kufuzu kombe la dunia 2018.
Hata hivyo timu ya taifa ya
Argentina ilionekana ikiwa kwenye hari ya hali ya juu mazoezini huku
mbwa akijiunga nao kwenye mazoezi.
Wachezaji wa Argentina wakifanya mazoezi na mbwa
Majeruhi Lionel Messi akiwa amekaa chini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni