.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 31 Agosti 2016

DK.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA

4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto, atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipeana mkono wa shukurani na Nd,Hassan Khatib Hassan,baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha ACP Sida Mohamed Himid kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitia saini hati ya kiapo ya ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
1
Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ walihudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi, walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
2
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
3
Baadhi ya Mawaziri wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi katika taasisi mbali mbali walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo. [Pica na Ikulu.] 31/08/2016.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni